Sunday, February 8, 2026
spot_img
HomeHabariTanzania ipo tayari kwa uwekezaji utakaoongeza thamani ya madini ndani ya nchi

Tanzania ipo tayari kwa uwekezaji utakaoongeza thamani ya madini ndani ya nchi

Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema Tanzania inakaribisha wawekezaji wote wa madini mkakati na kuweka msisitizo kwamba uongezaji thamani wa madini hayo mkakati lazima ufanyike Tanzania.

Mavunde ameyasema hayo leo Bali,Indonesia wakati wa majadiliano juu ya manufaa ya Madini Mkakati katika kukuza uchumi wa nchi wazalishaji ikiwa ni sehemu ya mkutano wa jukwaa la INDONESIA AFRIKA.

Waziri Mavunde ameonesha dhamira njema na mazingira mazuri yaliyowekwa na serikali chini ya uongozi wa Dk. Samia Hassan kuvutia uwekezaji nchini na hivyo kuwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika uchimbaji wa madini mkakati ambayo yana mahitaji makubwa duniani na Tanzania imebarikiwa nayo.

Waziri Mavunde alisisitiza kuwa kwasasa ni sharti la lazima kwamba madini mkakati hayo yaongezwe thamani nchini ili kuvutia viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo betri ya magari ya umeme.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments