Monday, May 18, 2026
spot_img
HomeHabariDk. Samia aanza kutekeleza mapendekezo Tume ya Jaji Chande, aunda Tume ya...

Dk. Samia aanza kutekeleza mapendekezo Tume ya Jaji Chande, aunda Tume ya uchunguzi Kijinai

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameanza rasmi kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kwa kuunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa matukio ya ghasia yaliyojitokeza katika kipindi hicho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Mei 18, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, tume hiyo imeundwa kwa lengo la kuchunguza kwa kina matukio ya vurugu, ghasia na ukiukwaji wa sheria uliotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Shabani Ally Lila ameteuliwa kuwa Kamishna na Mwenyekiti wa Tume hiyo.

Wajumbe wengine walioteuliwa katika tume hiyo ni Gad Mjemmas, Awadh Mohamed Bawazir pamoja na Aisheli Sumari ambao ni makamishna wa tume hiyo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments