Klabu ya Namungo FC imetangaza kuwasajili nyota wapya akiwemo beki wa zamani wa Simba, Hussein Kazi, aliyemaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi. Aidha, imemsajili Abdallah Mfuko kutoka Kagera Sugar na kipa Suleiman Said kutoka KVZ ya Zanzibar.

Namungo imeanza maandalizi ya msimu mpya huku ikiwa klabu iliyowaacha wachezaji wengi zaidi, jumla ya 13, akiwemo Antony Mlingo aliyejiunga na Simba na Salehe Karabaka aliyerejea baada ya mkopo. Wengine ni pamoja na Erasto Nyoni, Meddie Kagere, Emmanuel Asante, Issa Abushehe, Joshua Ibrahim, Erick Kapaito na wengine.
Klabu ya Pamba Jiji imefuatia kwa kuachana na wachezaji 11, wakiwemo Christopher Oruchum, Ladry Bakari, Deusa Kaseke, George Mpole na Modou Camara.




