Timu ya DB Lioness imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Dar es Salaam (BDL) 2025 kwa upande wa wanawake.
Kombe la ushindi lilikabidhiwa na Mkurugenzi wa Tehama wa Vodacom Tanzania PLC, Athumani Mlinga, katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Ushindi huo unaashiria ukuaji wa michezo ya wanawake nchini pamoja na jitihada za Vodacom kuendeleza vipaji na kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo.




