MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Abdul-Razaq Badru, amewaongoza wafanyakazi wa mfuko huo kutoa elimu ya hifadhi ya jamii na kuwahudumia wanachama kwenye Maadhimisho ya 4 ya Wiki ya Huduma za Fedha kwenye viwanja vya Ruanda-Nzovwe jijini Mbey, Oktoba 22, 2024.
Mwanachama wa PSSSF akifika kwenye banda hilo ataweza kupata taarifa za Michango yake, taarifa za Mafao, taarifa za uwekezaji, wastaafu wataweza kujihakiki lakini pia wote watapatiwa elimu ya matumizi ya PSSSF Kidijitali, ambapo mwanachama na mstaafu wanaweza kupata huduma zote kupitia simu janja au computer, ikiwemo kutuma madai.
Maonesho hayo yaliyobeba kaulimbiu isemayo “Elimu ya Fedha Msingi wa Maendeleo Kiuchumi.â€yameanza yanaendelea kwenye viwanja hivyo na yatafikia kilele Oktoba 26, 2024.




