Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeHabariSerikali yawahimiza wananchi kuwaunga mkono watu wenye ulemavu

Serikali yawahimiza wananchi kuwaunga mkono watu wenye ulemavu

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Ummy Nderiananga, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwaunga mkono Watu Wenye Ulemavu ili waweze kuendeleza na kuonyesha vipaji vyao katika maeneo mbalimbali.

Naibu Waziri Nderiananga alitoa wito huo leo jijini Dodoma, katika Ukumbi wa PSSSF, wakati wa uzinduzi wa Msimu wa Pili wa Mashindano ya Kusoma Qur’an kwa Watu Wenye Ulemavu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Lulida.

Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana na Watu Wenye Ulemavu bega kwa bega, kuhakikisha masuala yao yanapewa kipaumbele na kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu.

“Nimekuwa nikitembelea makundi mbalimbali ili kusikiliza changamoto zao na kuweka mikakati ya muda mfupi na mrefu kwa ajili ya kuzifanyia kazi,” alisema Naibu Waziri.

Aidha, aliipongeza Taasisi ya Lulida kwa kuanzisha mashindano hayo, akieleza kuwa ni hatua muhimu ya kutambua na kukuza vipaji na uwezo wa Watu Wenye Ulemavu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Lulida, Mhe. Hajjat Riziki Lulida, ametoa rai kwa vyombo vya habari kuendelea kuandika habari zinazojenga umoja, upendo na ushirikiano katika jamii.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments