Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeHabariRidhiwani Kikwete: “Niko tayari kuhojiwa kuhusu tuhuma za Lake Oil”

Ridhiwani Kikwete: “Niko tayari kuhojiwa kuhusu tuhuma za Lake Oil”

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amesema yuko tayari kuitwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ili kujibu tuhuma zinazomhusisha na umiliki wa vituo vya mafuta vya Lake Oil.

Akizungumza na watumishi wa wizara yake Novemba 26, 2025, Ridhiwani alisema uwazi kwa viongozi wa umma ni msingi muhimu wa utawala bora. Alisisitiza kuwa mara tu zinapojitokeza tuhuma au sintofahamu, ni wajibu wa mamlaka husika kufanya uchunguzi na kuweka ukweli wazi kwa umma.

“Malalamiko juu ya viongozi yamekuwa mengi; haijulikani lipi ni kweli na lipi si kweli. Ni muhimu uchunguzi ufanyike na taarifa zikawekwa wazi,” alisema.

Akimnukuu tukio la maandamano wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, Waziri Ridhiwani alisema baadhi ya wananchi walitoa malalamiko kuhusu maadili ya viongozi, ikiwamo madai kwamba vituo vya mafuta vya Lake Oil vinamilikiwa naye.

“Kuna mtu anaitwa Ali Edha ambaye anamiliki vituo vya mafuta vya Lake Oil, lakini vimechomwa moto kwa madai kuwa ni vya Ridhiwani,” alieleza.

Amesema Sekretarieti ya Maadili isiogope kumuita, kwani yuko tayari kuhojiwa wakati wowote. Aidha, amependekeza uchunguzi wa kina ufanyike na matokeo yake yatolewe hadharani kupitia mkutano na waandishi wa habari.

Pia aliishauri tume hiyo kuiomba jamii kutoa ushahidi wa ziada utakaowezesha kuthibitisha ukweli wa tuhuma hizo na kuweka suala hilo katika mtazamo sahihi kwa maslahi ya nchi na uongozi bora.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments