@cassypoolcapon, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kiuchumi kutoka Kenya, ameendelea kuitangaza na kuisifia Tanzania kama kivutio kinachoongoza kwa utalii wa safari barani Afrika, akibainisha kuwa nchi hiyo ina rasilimali za kipekee zinazoiweka katika nafasi ya juu ukilinganisha na mataifa mengine ya bara hilo.




