HomeGeneral NewsSamia: Kipimo chetu ni kuboresha maisha ya wananchi

Samia: Kipimo chetu ni kuboresha maisha ya wananchi

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kipimo kikuu cha viongozi Afrika si idadi ya matamko yanayotolewa, bali ni uwezo wa kuleta matokeo yanayoboresha maisha ya wananchi kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uwekezaji wenye tija.

Akizungumza leo Agosti 8, 2026 katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Africa50 na Jukwaa la Miundombinu kwa Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, Samia amesema Afrika sasa inapaswa kuelekeza nguvu katika utekelezaji wa maono yake ya maendeleo ili wananchi waone mabadiliko halisi.

Amesema Afrika haijawahi kukosa maono ya maendeleo, akitaja mipango mbalimbali ikiwemo Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika, Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) pamoja na mipango ya maendeleo ya kitaifa ambayo imeweka malengo makubwa ya kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.

“Hakuna ubishi kwamba wananchi wetu wanapima maendeleo si kwa matamko tunayoyatoa, bali kwa matokeo yanayoonekana kama vile barabara, nishati ya uhakika, bandari zenye ufanisi, reli, muunganiko wa kidijitali na miundombinu inayotengeneza ajira, kuvutia uwekezaji na kuboresha maisha,” amesema.

Akizungumzia Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo, amesema ni kutokana na kuongezeka kwa imani katika mageuzi yake ya kiuchumi, uwezo wa uwekezaji na nafasi yake ya kimkakati kama lango linalounganisha masoko ya Afrika. 

“Mkutano huu unaimarisha imani kwamba mustakabali wa Afrika utaongozwa na uongozi wa Waafrika, mitaji ya Afrika na ushirikiano wa Afrika,” amesema mkuu huyo wa nchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments