Wednesday, March 4, 2026
spot_img
HomeElimuCRDB yatoa Scholarships kwa watoto watatu Dar

CRDB yatoa Scholarships kwa watoto watatu Dar

DAR ES SALAAM- Wanafunzi watatu wa shule tofauti jijini Dar es Salaam washinda ufadhili wa masomo (school scholarships) kutoka Benki ya CRDB katika msimu wa pili wa tamasha la watoto lililoandaliwa na Kids’ Holiday Festival jijini hapa.

Mwaka huu Benki ya CRDB imeshirikiana na Kids’ Holiday Festival kutoa elimu ya fedha kwa watoto pamoja na wazazi au walezi wao tangu wakiwa wadogo, ili kuwajengea uwezo wa kusimamia masuala yao ya kiuchumi pindi watakapokuwa wakubwa. Elimu hii inatolewa katika matamasha yote mawili yanayoandaliwa na Kids’ Holiday Festival.

Katika tamasha la kwanza lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini hapa, akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Insurance Company, Wilson Mnzava amesema elimu ya fedha ni jambo nyeti kwa maendeleo ya kila mtu hivyo ni muhimu kujifunza mapema ili kurahisisha utekelezaji wa malengo binafsi.

“Jamii yetu inahitaji elimu ya fedha ili kutatua kwa urahisi changamoto zote zinazohusiana na masuala ya fedha. Nafurahi kuona tunatenga muda wa watoto kucheza na kujifunza mambo tofauti zikiwamo huduma za benki,” amesema Mnzava.

Ili kufikisha elimu ya fedha kwa watu wengi zaidi, Mnzava amesema Benki ya CRDB itaendelea kushirikiana na wadau wenye majukwaa yanayowakutanisha watoto kama ilivyo Kids’ Holiday Festival kuhakikisha inajenga msingi imara wa kuwaongezea washiriki maarifa kuhusiana na masuala ya fedha.

Katika tamasha hilo, Benki ya CRDB ilitoa zawadi ya ufadhili wa masomo (school scholarships) kwa watoto watatu, kama sehemu ya mchango wake katika kuunga mkono elimu na kuwahamasisha watoto kufikia ndoto zao kielimu.

“Nawapongeza watoto wote watatu walioshinda scholarships zetu leo na nawapongeza zaidi wazazi wao waliowatoa ili waje wajumuike na watoto wenzao katika tamasha hili,” amepongeza Mnzava ambaye aliongeza nafasi moja ya ufadhii kupitia CRDB Insurace Company ukiacha mbili zilizotolewa na Benki ya CRDB.

Walioshinda ufadhili huo wa masomo ni Gabriel Festo Joseph wa Shule ya Awali na Msingi Bubble Guppies na Arabella Ambonnye Mpangala wa Shule ya Msingi Mount Kibo, shule zote za jijini Dar es Salaam, pamoja na Alvin Freddy Urio wa Shule ya Sekondari Carmel ya mkoani Iringa.

Akizungumza baada ya ushindi wa mwanaye, mama mzazi wa Alvin aitwaye Pendo Peonson amesema kuna faida kubwa ya kuwapeleka watoto kwenye matamasha kwani licha ya kucheza huongeza maarifa ya elimu mbalimbali zinazotolewa pamoja na kutanua wigo wa marafiki.

“Nimekuja na Alvin pamoja na wadogo zake wawili. Ninafurahi mwanangu ameshinda lakini yeye hakuwa na akaunti ya benki ila leo tumefungua hapa. Nawasihi wazazi kuyatumia majukwaa haya kwani yana faida kwa watoto,” amesema Pendo.

Kwa upande wake, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kids’ Holiday Festival, Geraldine Mashele amesema tamasha hilo ni jukwaa muhimu kwa watoto kujifunza na kukuza vipaji vyao huku wakipata maarifa ya maisha ya baadaye.

“Tunafurahi kuona watoto wakifurahia na kujifunza kwa wakati mmoja. Ushirikiano wetu na Benki ya CRDB unatuwezesha kuwafikia watoto wengi zaidi na kuwajengea misingi itakayowasaidia kujisimamia kifedha wanapokua,” amesema Geraldine.

Geraldine ameongeza kuwa tamasha hilo ni sehemu ya mkakati mpana wa Kids’ Holiday Festival wa kuwajengea uwezo watoto na katika mipango ya baadaye wanatarajia kuanzisha klabu za watoto mashuleni zitakazowawezesha kujifunza kupitia michezo na shughuli nyingine shirikishi.

Tarehe 27 Desemba 2025 tamasha la pili la Kids’ Holiday Festival litafanyika Moshi mkoani Kilimanjaro, ambako ufadhili mwingine wa masomo utatolewa kwa watoto watakaojitokeja kushiriki.

Dar es Salaam. Wanafunzi watatu wa shule tofauti jijini Dar es Salaam washinda ufadhili wa masomo (school scholarships) kutoka Benki ya CRDB katika msimu wa pili wa tamasha la watoto lililoandaliwa na Kids’ Holiday Festival jijini hapa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments