Saturday, February 7, 2026
spot_img
HomeMichezo‎Simba yamkosa Nangu, Kagoma arejea

‎Simba yamkosa Nangu, Kagoma arejea

Klabu ya Simba imethibitisha kumkosa beki wa kati Wilson Nangu kwenye mchezo wa raundi ya tano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro de Luanda ya Angola, huku kiungo Yusuph Kagoma akirejea kikosini.

‎Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema Nangu ameendelea kubaki Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu, baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Esperance de Tunis. Kagoma naye alikuwa ameumia kwenye mchezo huo lakini sasa yuko tayari kurejea uwanjani.

‎Ahmed amesema licha ya Simba kuwa na nafasi ndogo ya kufuzu robo fainali, mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa klabu hiyo katika kulinda heshima yake kwenye michuano ya kimataifa.

‎Simba bado haijapata ushindi wowote kwenye Kundi D na inashika mkia, lakini imesisitiza itaingia uwanjani kupambana ili kumaliza mashindano kwa heshima.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments