Thursday, February 26, 2026
spot_img
HomeHabariZiara ya Faris Kagera yazaa matunda, serikali yatoa pongezi nzito

Ziara ya Faris Kagera yazaa matunda, serikali yatoa pongezi nzito

Waziri wa Vijana, Ajira na Maendeleo ya Ujuzi, Joel Nanauka, ameipongeza ziara ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Faris Buruhani, akisema imeleta hamasa mpya kwa vijana katika kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ya kiuchumi.

Akizungumza kwa njia ya simu, Waziri Nanauka amesema ameridhishwa na juhudi na ari kubwa inayooneshwa na vijana wa Kagera katika kushiriki miradi ya uzalishaji mali. Ameeleza kuwa ushiriki huo ni ishara ya mabadiliko chanya yanayolenga kujenga uchumi imara kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Amebainisha kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa uwekezaji na ujasiriamali, akiwataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa. 

Amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali chini ya uongozi wa Rais **Samia Suluhu Hassan** ni kuwawezesha vijana kuwa kitovu cha mapinduzi ya kiuchumi kupitia mikopo, mafunzo ya stadi na mitaji, badala ya kubaki wasikilizaji wa sera bila kuchukua hatua.

Kwa upande wake, Buruhani yupo katika ziara ya siku nane mkoani Kagera, akitembelea na kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kufanya mikutano na vijana katika wilaya mbalimbali. 

Ziara hiyo inalenga kuhamasisha uwajibikaji, ubunifu na ushiriki wa moja kwa moja wa vijana katika miradi ya uzalishaji mali ili kuongeza kipato na kuchochea maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments