Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iliamua kufuata mfumo wa kidemokrasia hivyo inaendelea kujifunza na kukua kupitia mfumo huo.
Dkt Samia ameeleza hayo leo Aprili 23,2026 wakati akipokea ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu Amani Oktoba 29, iliyotoa matokea yake leo Ikulu Dar es Salaam.
“Nakumbuka Mwalimu Nyerere katika hotuba yake akiwa kula Rio de Janerio (Brazil) hapa namnukuu kuwa demokrasia sio chupa ya ‘coca cola’ ambayo unaweza kuiagiza, hivyo inapaswa kulingana na nchi kuendelezwa,”
“Kwa maneno mengine demokrasia haina budi kujengwa kwa kufuata mazingira ya nchi, na muhimu zaidi mila na desturi za nchi husika. Sasa nasi kama nchi tuachwe tujenge demokrasia yetu kwa misingi yetu mila na desturi zetu,” amesema. #RipotiYaTume #UkweliOkt29




