Monday, April 27, 2026
spot_img
HomeHabariPSSSF yatoa huduma banda kwa banda Maonesho ya Muungano, Zanzibar

PSSSF yatoa huduma banda kwa banda Maonesho ya Muungano, Zanzibar

Zanzibar Aprili 26, 2026- Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kupitia watumishi wake wanaotoa huduma kwenye Maonesho ya Muungano wa miaka 62, kwenye viwanja vya Mao Ze Dong, mjini Unguja, leo Aprili 26, 2026, wamepita banda kwa banda ili kutoa elimu na kuhudumia wanachama wake.

‎Zoezi hilo liliongozwa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Zanzibar,  Mariam Saleh ambapo pamoja na kuwahudumia walieleza jinsi PSSSF ilivyofanya maboresho katika utoaji wa huduma na mafao.

‎“ Hatua hii ni kutoa fursa ya kuwahudumia wanachama wetu ambao wanakosa muda wa kutembelea kwenye banda letu kutokana na wao kutoa huduma kwenye mabanda ya taasisi zao,” alibainisha Mariam.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments