Zanzibar Aprili 26, 2026- Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kupitia watumishi wake wanaotoa huduma kwenye Maonesho ya Muungano wa miaka 62, kwenye viwanja vya Mao Ze Dong, mjini Unguja, leo Aprili 26, 2026, wamepita banda kwa banda ili kutoa elimu na kuhudumia wanachama wake.

Zoezi hilo liliongozwa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Zanzibar, Mariam Saleh ambapo pamoja na kuwahudumia walieleza jinsi PSSSF ilivyofanya maboresho katika utoaji wa huduma na mafao.
“ Hatua hii ni kutoa fursa ya kuwahudumia wanachama wetu ambao wanakosa muda wa kutembelea kwenye banda letu kutokana na wao kutoa huduma kwenye mabanda ya taasisi zao,” alibainisha Mariam.






