Monday, April 27, 2026
spot_img
HomeHabariTanzania yashiriki Mkutano Nishati, Uchukuzi

Tanzania yashiriki Mkutano Nishati, Uchukuzi

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Wizara ya Uchukuzi imeshiriki Mkutano wa 5 wa Kamati Maalum ya Wataalamu ya Umoja wa Afrika kuhusu Uchukuzi na Nishati (STC), unaofanyika jijini Johannesburg.

Ushiriki wa Tanzania unaongozwa na Mhandisi Innocent Luoga, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, ambaye ameongoza ujumbe wa wataalamu katika majadiliano ya kimkakati ya kuimarisha miundombinu ya nishati na uchukuzi barani Afrika.

Wataalamu wengine walioshiriki ni pamoja na Stella Katondo, Mkurugenzi wa Usalama wa Usafiri na Mazingira, na Mohamed Salum, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).

Mkutano huo unaofanyika kuanzia Aprili 27 hadi 29, 2026, unajadili masuala muhimu ikiwemo kuongeza uwekezaji katika nishati jadidifu, matumizi ya gesi asilia, na kuimarisha miundombinu ya umeme wa kuvuka mipaka.

Aidha, kikao cha Mawaziri kinatarajiwa kufanyika Aprili 30, 2026, ambapo Tanzania pia itashiriki katika ngazi ya juu zaidi.

Kwa ujumla, nchi wanachama zinajadili mikakati ya kuboresha upatikanaji wa nishati ya uhakika na nafuu pamoja na kuendeleza mifumo jumuishi ya uchukuzi kama reli, barabara, anga na usafiri wa majini ili kurahisisha biashara na usafirishaji barani Afrika.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments