Afisa Mtendaji Mkuu wa SanlamAllianz Life Insurance, Julius Magabe, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Salama Plan bidhaa mpya inayolenga kuwahudumia wastaafu na wanaokaribia kustaafu kupata uhakika wa kipato. Tukio limefanyika Aprili 23, 2026, katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa SanlamAllianz Life Insurance,Julius Magabe, amezindua rasmi bidhaa mpya ya Salama Plan, inayolenga kuwahudumia wastaafu na wale wanaokaribia kustaafu kutoka sekta binafsi, sekta za umma pamoja na wajasiriamali, ili waweze kuwa na uhakika wa kipato wanapostaafu.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Magabe alieleza kuwa mpango huo unalenga kupunguza wasiwasi wa kipato kwa wastaafu. Tukio hilo pia limeshuhudiwa na Mkurugenzi wa Biashara wa SanlamAllianz Tanzania, Kyenekiki Kyando, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Actuarial, Mary Murya.
Hafla hiyo imefanyika Aprili 23, 2026, katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.




