Thursday, April 30, 2026
spot_img
HomeHabariMchome wa akemea siasa za matusi

Mchome wa akemea siasa za matusi

Lembrus Mchome amesema CHADEMA kinapaswa kubaki kuwa chama cha Watanzania wote na si jukwaa la matusi, akionya kuwa lugha ya kejeli na dharau haiwezi kujenga umoja wala kuimarisha siasa za maendeleo.

Amesema kwa sasa hali imebadilika na kushuhudiwa kuongezeka kwa matusi kutoka kwa makundi mbalimbali, bila kujali umri au nafasi za viongozi, jambo linalowaumiza wanachama wengi na kupunguza heshima ya chama.

Mchome ameongeza kuwa ni muhimu kwa viongozi kuwa mfano bora kwa kauli na matendo, akisisitiza kuwa siasa za hoja na staha ndizo zinazoweza kuijenga jamii na kuimarisha demokrasia.

Akirejea kauli ya hivi karibuni ya John Heche aliyewataka wanasiasa kuacha matusi, Mchome amesema kauli hiyo inapaswa kuambatana na vitendo, akidai kuwa hapo awali Heche aliwahi kuwaita baadhi ya wenzake “vikaragosi.”

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments