Thursday, April 30, 2026
spot_img
HomeMichezoCP Awadhi akagua miundombinu na mifumo ya usalama Uwanja wa AFCON Arusha

CP Awadhi akagua miundombinu na mifumo ya usalama Uwanja wa AFCON Arusha

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi (CP) Awadh Juma amefika Jijini Arusha kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa miundombinu pamoja na mifumo ya kiusalama katika uwanja unaojengwa kwa ajili ya mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).

Katika ukaguzi huo, CP Awadh amepitia maeneo mbalimbali ya uwanja huo, ikiwemo mifumo ya usalama pamoja na eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi ndani ya uwanja huo.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha usalama unaimarishwa wakati wote, kabla na baada ya mashindano hayo muhimu kwa bara la Afrika.

Aidha, amesisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kuendelea kudumisha sifa nzuri iliyojengwa na waasisi wa Tanzania waliohubiri amani na utulivu, huku akiwaomba wananchi kuwapokea vyema wageni watakaofika kutoka mataifa mbalimbali kushuhudia mashindano ya AFCON.

Katika ziara hiyo ya ukaguzi, CP Awadh aliambatana na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Zauda Mohamed, pamoja na Mkuu wa Operesheni za Polisi Mkoa wa Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Oscar Felician.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments