HomeAfyaRC Batilda apongeza ubunifu wa wanafunzi MUHAS

RC Batilda apongeza ubunifu wa wanafunzi MUHAS

TANGA: Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Buriani, amepongeza bunifu zinazotengenezwa na wanafunzi na watafiti wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), akisema zinasaidia kutatua changamoto za jamii, hususan katika sekta ya afya.

Balozi Batilda ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la MUHAS katika maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika Shule ya Sekondari Usagara mkoani Tanga.

Amesema amefurahishwa na namna MUHAS inavyowawezesha vijana kutumia elimu na ujuzi wao kubuni suluhisho zinazolenga kukidhi mahitaji halisi ya jamii.

Ushiriki wa MUHAS katika maadhimisho hayo unawawezesha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali kujifunza kuhusu bunifu na teknolojia zinazozalishwa chuoni, pamoja na kuelewa mchango wa elimu, utafiti, ujuzi na ubunifu katika maendeleo ya Taifa.

Kupitia maadhimisho hayo, MUHAS inaendelea kuimarisha juhudi za kuibua, kukuza na kuendeleza bunifu zinazolenga kutatua changamoto za jamii, hasa katika huduma za afya.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments