HomeHabariMfuko wa Bima ya Afya kwa Wote kunufaika na mabadiliko ya Sheria...

Mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote kunufaika na mabadiliko ya Sheria za Kodi 2026/27


NKASI, Rukwa:
 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema marekebisho ya sheria za kodi yaliyoanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2026/27 yanalenga kuongeza mapato ya Serikali yatakayosaidia kugharamia utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote nchini.

Akizungumza katika semina kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Afisa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa TRA, Yusta Kaunda, amesema miongoni mwa mabadiliko hayo ni ongezeko la ushuru wa bidhaa wa Shilingi 20 kwa kila sigara 1,000.

Kaunda amesema ongezeko hilo ni sehemu ya marekebisho yaliyofanywa kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2026, ambayo pia imehusisha marekebisho yanayohusiana na Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, Sura ya 161.

Amesema mapato yatakayokusanywa kutokana na ongezeko hilo la ushuru yameelekezwa kuwa chanzo maalum cha fedha kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote.

Kwa mujibu wa Kaunda, hatua hiyo inalenga kuongeza uwezo wa Serikali kugharamia huduma za afya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma hizo kwa ufanisi zaidi.

Aidha, amesema marekebisho hayo yameunganisha utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote na sheria zinazosimamia ushuru wa bidhaa, ikiwemo Sheria ya Ushuru, Sura ya 147, ili kuweka mfumo wa kisheria wa ukusanyaji na uelekezaji wa mapato hayo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wafanyabiashara Wilaya ya Nkasi, Willington Kiziba, ameishukuru TRA na Serikali kwa ujumla kwa maboresho hayo ya sheria, akisema yana umuhimu katika kuongeza mapato na kuchangia huduma zinazogusa maisha ya wananchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments