Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariMwenyekiti wa CHADEMA Mwanga aita waandishi kuzungumza leo

Mwenyekiti wa CHADEMA Mwanga aita waandishi kuzungumza leo

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jimbo la Mwanga, mkoani Kilimanjaro, Lembrus Mchome, anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari leo saa 5 asubuhi, jijini Arusha.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo utatoa picha ya kinachoendelea katika chama chake, ukiwepo mpango wa kufukuzwa na viongozi wa juu wa chama hicho kufuatia ukiukwaji mkubwa wa chama hicho uliofanywa katika Uchaguzi Mkuu sanjari na uteuzi wa viongozi watano wa Kamati Kuu wa Chadema.

Mchome anatoka hadharani kuzungumzia jinsi viongozi hao wa Chadema, chini ya Mwenyekiti wa Taifa Tundu Lissu na Makamu wake John Heche, walivyoamua kusigina Katiba yao, huku wakikataa kukosolewa na wanachama wanaotofautiana kimtazamo.

Lissu na viongozi wenzake wa Chadema wamejinasibu kama moja ya watu wanaopenda kuikosoa serikali, licha ya wao kushindwa kuvumilia wanapokosolewa katika uendeshaji wa chama chao.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments