Sunday, March 8, 2026
spot_img
HomeBiasharaNMB yadhamini kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi Wakuu wa...

NMB yadhamini kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi Wakuu wa taasisi za umma 2025

Benki ya NMB imedhamini na kushiriki kikamilifu katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi Wakuu wa Taasisi za Umma (CEOs Forum 2025) kinachoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC).

Ujumbe wa NMB kwenye kikao hicho umeongozwa na David Nchimbi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, akishirikiana na Juma Kimori, Afisa Mkuu wa Fedha na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu.

Viongozi Zaidi ya 650 Washiriki

Kikao kazi hicho cha siku tatu kimekusanya zaidi ya viongozi 650 kutoka Taasisi, Mashirika na Wakala wa Serikali, kikilenga kujadili changamoto, fursa na mustakabali wa taasisi za umma katika kukuza maendeleo ya taifa.

Kaulimbiu ya Kikao Kazi

Kauli mbiu ya CEOs Forum 2025 ni:

“Kujenga Ushirikiano Endelevu katika Mazingira ya Ushindani wa Kimataifa – Wajibu wa Mashirika ya Umma.”

Kupitia ushiriki huu, NMB imeonesha dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na Serikali na taasisi zake katika kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments