Saturday, March 7, 2026
spot_img
HomeHabariMpina akwama kurejesha fomu, azuiwa getini kuingia INEC

Mpina akwama kurejesha fomu, azuiwa getini kuingia INEC

Mgombea urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, amezuiwa kuingia katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) jijini Dodoma, alipokuwa akielekea kurejesha fomu za kugombea nafasi hiyo.

Mpina alifika makao makuu ya INEC saa 6:40 mchana, akiwa ameambatana na wanachama wa chama chake. Hata hivyo, wote walizuiwa kuingia ndani ya geti la tume hiyo, hali iliyozua maswali kutoka kwa wafuasi wake waliotaka kufahamu sababu ya kuzuiliwa.

Baada ya muda, walielezwa kuwa vyama vilivyotakiwa kurejesha fomu ni 17 pekee, ambapo ACT-Wazalendo haikuwemo kwenye orodha hiyo. Askari waliokuwa getini waliwaeleza wafuasi hao kusubiri majibu kutoka INEC, huku wakimshauri Mpina kubaki ndani ya gari lake akisubiri hatma.

Wanachama hao walitii maelekezo hayo na kusogea mita chache kutoka geti la INEC, ambapo kulikuwepo ulinzi mkali ndani na nje ya eneo hilo. Pamoja na sintofahamu iliyojitokeza, wafuasi wa ACT waliendelea kufuata maelekezo ya askari waliokuwa wakisimamia ulinzi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments