Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inawajali wananchi wa hali ya chini, ndio manaa inajenga miundombinu mbalimbali inayowaletea maendeleo.
Dk. Samia ameeleza hayo leo Jumamosi Septemba 6,2025 wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kunadi vipaumbele vya Ilani ya CCM ya uchaguzi kwa mwaka 2025/30 mkoani Iringa.
Kabla ya kueleza hayo, Dk. Samia alisema kabla ya kuanza kwa kampeni alikutana katika kikao cha wazee kilichofanyika jijini Dodoma, ambapo alielezwa yeye Serikali yake si ya wanyonge.
“Niliita wazee wa mikoa mbalimbali kwa uwakilishi wao. Nilizungumza nao jambo moja kubwa kwamba ambalo nataka nilirudie hapa,”
Amesema alizinduliwa kampeni mkoani Dar es Salaam, akapita Morogoro, Dodoma, Songwe, Mbeya, Njombe leo amefika Iringa, na kwamba mambo yote yanayozungumzwa ni yanayomgusa wananchi wanaoishi vijijini.
“Lakini niliwaambia wazee siongozi wanyonge bali naongoza na kuwatengenezea Tanzania wanayoitaka. Yote yaliyosemwa, yatakayosemwa yamemgusa Mtanzania wa chini kabisa, umeme upo katika vijijini unakwenda kwenye vitongoji,”
“Maji yanachotwa kwenye bomba vijijini, zahanati na vituo vya afya pamoja na vipimo vya maana vipo wilayani na vijijini,” amesema Dk Samia nakuongeza kuwa
“Shule nzuri zimejengwa vijijini, nilipopita Songwe niliambiwa kuna shule za ghorofa zimejengwa, maana mtoto wa wakulima.Huku ndiko kumjali mnyonge, sio lazima usimame useme unajali wanyonge, kumjali mnyonge ni kufanya maendeleo yanayomgusa hasa ngazi ya chini,” amesema.









