Saturday, March 7, 2026
spot_img
HomeHabariMtoto afariki kwa kupigwa na wazazi wake akituhukiwa kuiba TV

Mtoto afariki kwa kupigwa na wazazi wake akituhukiwa kuiba TV

Mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Bright Joel (15), mkazi wa Mtaa wa Igodima katika Kata ya Iganzo jijini Mbeya, amefariki dunia baada ya kupigwa na wazazi wake wakimtuhumu kuiba televisheni nyumbani kwao.

Kwa mujibu wa taarifa za majirani wa familia hiyo, tukio hilo lilitokea juzi jioni ambapo wazazi wa kijana huyo wanadaiwa kumshushia kipigo kikali na kisha kumtelekeza ndani akiwa na hali mbaya, kabla ya kutokomea kusikojulikana.

Inadaiwa kuwa majirani waligundua hali hiyo kesho yake na kubaini kuwa kijana huyo alikuwa ametupwa ndani ya nyumba huku akiwa na hali mbaya. Walichukua hatua ya kumkimbiza hospitalini kwa ajili ya matibabu, lakini taarifa zinaeleza kuwa hakuweza kupona na hatimaye alifariki dunia.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments