Mashindano ya Ligi ya Muungano ya Netiboli yanatarajiwa kufanyika Novemba 20–28, 2025, Visiwani Zanzibar, yakihusisha timu nane — nne kutoka Tanzania Bara na nne kutoka Zanzibar.
Mwenyekiti wa CHANETA, Devotha Marwa, alisema maandalizi yanaendelea vizuri huku timu zikikamilisha usajili na kujiandaa kutetea ubingwa.
“Tunataka kuendelea kulimiliki kombe la ubingwa. Kila timu ijipange vyema kwa mashindano haya yatakayokuwa na ushindani mkali,” alisema Marwa.




