Tuesday, March 10, 2026
spot_img
HomeMichezoSimba SC yaendelea kuitesa JKT Tanzania Ligi Kuu

Simba SC yaendelea kuitesa JKT Tanzania Ligi Kuu

Timu ya Simba SC imeendeleza ubabe wake dhidi ya JKT Tanzania baada ya kupata ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa leo, na kuendeleza rekodi yake bora ya ushindi dhidi ya wanajeshi hao katika misimu ya hivi karibuni.

Takwimu zinaonesha kuwa JKT Tanzania imepata bao lao la kwanza dhidi ya Simba SC ndani ya mechi saba (7) zilizopita katika Ligi Kuu, jambo linaloonesha jinsi ambavyo Simba imekuwa ikidhibiti mchezo kila wanapokutana. Katika mechi hizo saba, Simba imefunga jumla ya mabao 14, huku JKT ikipata bao moja pekee.

Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, timu hizo zimekutana mara 11 kwenye ligi, ambapo Simba imeshinda mechi 10 na JKT Tanzania ikishinda mchezo mmoja pekee. Hadi kufikia mechi ya leo, Simba SC imekuwa ikishinda mechi saba (7) mfululizo dhidi ya JKT Tanzania – rekodi inayodhihirisha tofauti kubwa ya ubora kati ya vikosi hivyo viwili.

Katika msimu uliopita wa Ligi Kuu, JKT Tanzania ilipoteza michezo yote miwili dhidi ya Simba kwa matokeo ya bao 1-0. Mchezo wa kwanza uliochezwa away kwa JKT ulimalizika kwa bao la penati lililofungwa na mchezaji “Usiku”, huku mchezo wa marudiano pia ukimalizika kwa bao la Isamuhyo lililopatikana katika dakika za mwisho za kipindi cha pili.

Kwa matokeo haya na takwimu hizi, Simba SC inaendelea kuwa tishio kwa JKT Tanzania kila wanapokutana, huku mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi wakiendelea kufurahia mwenendo imara wa timu yao kwenye kampeni za msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments