Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeBiasharaMkurugenzi Mkuu TALIRI akagua maendeleo mradi wa kuku Horasi Mtwara

Mkurugenzi Mkuu TALIRI akagua maendeleo mradi wa kuku Horasi Mtwara

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Prof. Erick Komba, ametembelea Kituo cha TALIRI Naliendele kilichopo Mtwara, Kanda ya Kusini, kwa ajili ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Uzalishaji wa Kuku wa Aina ya Horasi unaotekelezwa kituoni hapo.

Akiwa katika ziara hiyo, Prof. Komba aliupongeza uongozi wa kituo hicho, akiongozwa na Mkurugenzi wa TALIRI Kanda ya Kusini, Dk. Fadhili Guni, kwa usimamizi mzuri wa mradi huo. Alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mradi unaendelea kufanyika kwa kufuata mpango kazi uliowekwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Aidha, Prof. Komba alishauri kituo hicho kuangalia uwezekano wa kupanua wigo wa tafiti zake, ili kuongeza tija na mchango wake katika kukuza sekta ya mifugo nchini.

Kwa upande wake, Dk. Guni alieleza kuwa mradi huo wa kuku wa Horasi kwa sasa upo katika hatua ya kuzalisha kizazi cha pili, huku lengo likiwa ni kufikia kizazi cha sita ambacho kitawezesha upatikanaji wa Horasi halisi.

Alifafanua kuwa mradi huo unalenga kuzalisha kuku wa asili mwenye uwezo wa kutaga mayai yasiyopungua 200 kwa mwaka na kufikia uzito wa kilo 1.5 ndani ya kipindi cha wiki 16, sawa na miezi minne.

Dk. Guni aliongeza kuwa baada ya kukamilika kwa mradi huo, matarajio ya TALIRI ni kuhakikisha kuku wa Horasi wanawafikia wafugaji kote nchini, ili kusaidia kuongeza uzalishaji na kipato cha wafugaji wa kuku wa asili.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments