Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan,amemuapisha Dkt Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu, akimweleza uteuzi wake umepitia ushindani mkubwa.
Hata hivyo, Dk Samia amesema licha ya kuwa na ushindani mkubwa, lakini katika vigezo kadhaa, Dk Mwigulu amewashinda wenzake kwa sifa kidogo kuliko wengine alioshindana nao.
Dk Samia ameeleza hayo, leo Ijumaa Novemba 14, wakati akimuapisha Waziri Mkuu mpya, Dk Mwigulu Nchemba aliyemteua jana na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hafla ya kumuapisha Dk Mwigulu imefanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodomo na kuhudhuriwa na viongozi wakuu waandamizi wa Serikali na wastaafu.
“Vigezo vyote vilivyopimwa, tumepima katika maeneo mbalimbali vya kuitumikia nchi hii na kulitumikia Taifa hili. Kubwa zaidi ni kuwatumikia wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”




