Golikipa wa Simba SC, Moussa Camara, amefanyiwa upasuaji wa goti nchini Morocco baada ya jeraha lililokuwa likimsumbua kwa muda. Upasuaji huo uliofanyika Jumanne, Novemba 18, 2025, umekamilika kwa mafanikio na umeelezwa kuwa umeenda vizuri bila changamoto zozote za kiafya.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu, Camara atarudi uwanjani baada ya wiki nane hadi kumi, hatua inayomaanisha Simba italazimika kuendelea na kampeni zake za ligi na michuano ya kimataifa bila huduma ya mlinda mlango huyo namba moja kwa kipindi hicho.
Inaelezwa kuwa benchi la ufundi la Simba linaandaa mipango mbadala kuhakikisha safu ya ulinzi inabaki imara wakati Camara akiendelea na matibabu na programu ya kurejea kwenye ubora wa kawaida.






