Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema licha ya changamoto zinazoendelea ulimwenguni, Serikali inafanya kila linalowezekana ili Watanzania wabaki katika hali salama ya maisha.
Dkt Samia ameeleza leo Ijumaa Mei Mosi, 2026 katika hotuba yake wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’, yaliyofanyika kitaifa mkoani Njombe.
“Kama mnavyosikia huko duniani mambo ni makubwa, kuna mambo ambayo kwa vyovyote viule yanaathiri chumi za dunia hasa nchi zinazoendelea, hivyo kwa vyovyote lazima tukae kitako au kukabiliana na hali inayobadilika.
“Na hili nilifafananishe na yale yaliyosema na mbunge kuwa Serikali ina mpango gani, nataka niseme ule ugumu unaanza Serikalini kwanza, halafu unakwenda kwa wengine.Kwa hiyo kwa ugumu huo huo Serikali tunaendelea kufanya majambo ya kuhakikisha Watanzania wanabaki na kiwango cha maisha tulichonacho au ikibidi mambo yawe mazuri zaidi, tunajitahidi tusirudi chini,” amesema.




