Mashahidi walioshiriki kufanya ghasia waliokuja mbele ya tume na kukiri kwamba baadhi yao walipewa simu maalumu za mkononi na kupewa kazi ya kupiga picha na video za matukio kama vile majeruhi na vifo au kupiga picha jirani na magari ya jeshi la ulinzi sambamba na picha za maeneo mbalimbali ya wafanya ghasia waliokuwa wamefanikiwa kufanya uratibu,” Jaji Othman Chande.
“Kuna baadhi ya watu walipewa simu kwa ajili ya kupiga picha za vurugu na kusambaza katika mitandao ya kijamii ili kuibua hasira za wananchi kufanya ghasia wakiaminishwa kwamba Jeshi liko upande wao,” Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Jaji Chande Othman.




