Saturday, November 8, 2025
spot_img
HomeHabariRais Samia: Baadhi ya waliokamatwa kuivuruga amani wanatoka nje ya Tanzania

Rais Samia: Baadhi ya waliokamatwa kuivuruga amani wanatoka nje ya Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kati ya waliokamatwa kuhusika katika matukio la uvunjifu wa amani na uharibifu wa miundombinu nchini, wapo wanaotoka nje ya Tanzania.

Amesema kilichotokea hakiendani na taswira na sifa za Kitanzania na hivyo, kilichofanywa wala si Utanzania.

Dkt. Samia ametoa kauli hiyo, Jumatatu Novemba 3, 2025 katika hotuba yake mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania kwa kipindi cha pili.

“Kilichotokea hakiendani na taswira na sifa za Kitanzania na wala sio Utanzania. Haikutushangaza kuona kuwa baadhi ya vijana waliokamatwa kutokana na kadhia hiyo wanatoka nje ya Tanzania,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments