Saturday, November 8, 2025
spot_img
HomeBiasharaRC Mrindoko aonya wa'biashara wanaopandisha bei baada ya uchaguzi

RC Mrindoko aonya wa’biashara wanaopandisha bei baada ya uchaguzi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara mkoani humo dhidi ya kutumia kipindi cha baada ya uchaguzi kama kisingizio cha kupandisha bei za bidhaa.

Amesisitiza kuwa shughuli zote za biashara zinapaswa kuendelea kama kawaida, huku bidhaa zenye bei elekezi zikiuzwa kwa viwango vilivyowekwa rasmi na serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, RC Mrindoko alisema huduma muhimu kama elimu, afya, usafiri, biashara, masoko na vituo vya mafuta zinapaswa kuendelea kutolewa bila usumbufu wowote ili wananchi waendelee kupata mahitaji yao ya kila siku bila changamoto.

Amesema serikali haitavumilia kuona wafanyabiashara wachache wakitumia visingizio vya kisiasa au mabadiliko ya kipindi cha uchaguzi kuongeza bei kiholela, hatua ambayo inaweza kuathiri ustawi wa wananchi.

Shughuli za kiuchumi lazima ziendelee kama kawaida. Hatutaruhusu bei za bidhaa kupanda kiholela kwa sababu ya uchaguzi. Serikali ipo makini kufuatilia hali hii,” alisema Mrindoko.

Ameongeza kuwa ofisi yake itaendelea kufuatilia kwa karibu upatikanaji wa bidhaa na huduma muhimu, kuhakikisha hakuna ongezeko holela la bei na kuwa wananchi wanapata huduma bora kwa gharama nafuu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments