Friday, May 15, 2026
spot_img
HomeBiasharaVipaumbele tisa vyatajwa Bajeti ya Maliasili na Utalii 2026/2027

Vipaumbele tisa vyatajwa Bajeti ya Maliasili na Utalii 2026/2027

📌 Uhifadhi, Miundombinu na Utalii vyapewa kipaumbele

Wizara ya Maliasili na Utalii imewasilisha Bungeni Hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027, na kutaja vipaumbele vitakavyotekelezwa kwenye bajeti hiyo.

Akiwasilisha Bungeni mjini Dodoma Mei 15,2026, Waziri wa Wizara hiyo Dk. Ashatu Kijaji amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na Kuimarisha uhifadhi, ulinzi, na matumizi endelevu ya rasilimali za wanyamapori, misitu, nyuki na malikale, Kuimarisha miundombinu wezeshi katika maeneo ya utalii na hifadhi ikiwemo barabara, viwanja vya ndege, mawasiliano na huduma za kijamii.

Vipaumbe vingine ni Kuimarisha utangazaji utalii ndani na nje ya nchi kwa kutumia mikakati mahsusi ikiwemo masoko ya Mashariki ya Mbali na Mashariki ya Kati, na kutumia fursa ya AFCON 2027, IPU, Mashindano ya ulimbwende ya dunia, utoaji wa tuzo za ubora kuhusu masuala ya utalii zinazoandaliwa na WTA matukio yatakayofanyika nchini.

Ameongeza kuwa vipaumbele vingine ni Kuendeleza na kuboresha mazao ya utalii ya kimkakati ikiwemo utalii wa meli, mikutano na matukio (MICE); pamoja na kutambua na kusajili mazao mapya, Kuimarisha uzalishaji, uongezaji thamani na masoko ya mazao ya misitu na nyuki, Kuimarisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika usimamizi wa rasilimali, ulinzi, ufuatiliaji, ukusanyaji wa mapato, pamoja na utangazaji wa utalii.

Aidha, Dk.Kijaji maeneo mengine ni Kuimarisha Utafiti, Ubunifu na Maendeleo ya Rasilimaliwatu; na Kufanya mapitio ya Sera, Sheria, Kanuni na miongozo ili kuendana na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia na Kuboresha mazingira ya kazi, mifumo ya usimamizi wa utendaji na uwajibikaji.

Pia Dk. Kijaji amesema ili vipaumbele hivyo viweze kutekelezwa, ameliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha Shilingi Bilioni 334 kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments