HomeElimuWanafunzi Mpwapwa wanufaika na elimu ya afya ya hedhi, ushirikishwaji

Wanafunzi Mpwapwa wanufaika na elimu ya afya ya hedhi, ushirikishwaji

Katika Shule ya Msingi Chilendu wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma wanafunzi 200 wameshiriki kikao cha utoaji elimu ya uelewa kuhusu afya ya hedhi na madhara ya unyanyapaa.

Akizungumza katika kikao hicho cha kuhamasisha afya na usafi wa hedhi kilichofanyika wilayani humo hivi karibuni, Ofisa kutoka Shirika la Water for People Tanzania, Emmanuel Mashana alisema: “Tulishuhudia kujiamini kukijengwa, sauti zikipewa nguvu, na vikwazo vikivunjwa.”

Mashana, alisema kuwa shirika hilo lilitoa taulo za kike za matumizi ya mara moja kwa wasichana balehe na kuunda mazingira salama na yenye msaada ambapo mazungumzo kuhusu hedhi, usafi, heshima na ushirikishwaji yaliweza kufanyika kwa uwazi bila aibu.

Mashana aliongeza kuwa zaidi ya wanafunzi 200 walishiriki, wakiwemo wavulana, wasichana na watoto wenye ulemavu, jambo lililoonesha kuwa mabadiliko ya kweli huanza pale kila mtu anaposhirikishwa katika mazungumzo.

Alisema afya ya hedhi si suala la wasichana pekee, bali ni kuhusu elimu, huruma, usawa na kujenga jamii ambazo kila mtoto anahisi kuheshimiwa, kuelimishwa na kuungwa mkono.

“Tukio hili limetukumbusha kuwa msichana mwenye kujiamini hubaki shuleni, mvulana mwenye uelewa huwa mshirika mzuri, mtoto mwenye ulemavu anastahili kupata heshima na taarifa sawa, na jamii inayosikiliza ina uwezo wa kubadilisha mustakabali wa baadaye,” alisema ofisa huyo.

Afisa Afya wa Wilaya, Mary Mabango alisema wanafunzi wamefundishwa kuwa ushirikishwaji ni muhimu, unyanyapaa una madhara, na uelewa una nguvu ya kubadilisha maisha.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments