“Umekuwa utaratibu wetu wa kila mwaka kutoa msaada kama huu kwenye vituo vya kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na tunaomba jamii iige mfano wa St Anne Marie Academy,” alisema
“Shule yetu imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya kitaifa kuanzia shule ya awali, msingi na sekondari, tunafaulisha na kuwa wa kwanza kitaifa, kiwilaya na hata kwenye kata kwa hiyo mafanikio yote haya lazima turudishe shukrani kwa jamii kwa kutoa misaada kama hii,” alisema
Alisema shule hiyo itaendelea kutoa elimu bora kwa kuhakikisha wanafunzi wake wanaendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa kuanzia ngazi ya Kata.
“Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ilivyoweka mazingira mazuri kwenye sekta ya elimu na kuwa karibu na wawekezaji binafsi katika elimu hali ambayo imechangia sekta ya elimu kuendelea kukua,” alisema
Mmoja wa watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho, Edina John alishukuru wanafunzi wa St Anne Marie Academy kwa msaada huo na kuomba jamii kuiga mfano huo.
Alisema watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wanamahitaji mengi hivyo hatua ya wanafunzi wa shule hiyo kuamua kuwapelekea msaada imewafariji na kuona kwamba jamii inawajali.




