Tuesday, March 24, 2026
spot_img
HomeHabariTanzania kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Madini Zambia

Tanzania kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Madini Zambia

Serikali kupitia Wizara ya Madini imetangaza ushiriki wake katika mkutano wa 13 wa kimataifa wa madini na nishati unaojulikana kama Zambia International Mining and Energy Conference (ZIMEC 2026), utakaofanyika tarehe 25 hadi 26 Machi 2026 nchini Zambia.

Naibu Waziri wa Madini, Steven Kiruswa, anatarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika mkutano huo muhimu unaolenga kujadili fursa za uwekezaji, maendeleo ya sekta ya madini na nishati, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa.

Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo unalenga kukuza mahusiano ya kiuchumi, kubadilishana uzoefu, na kuvutia wawekezaji zaidi katika sekta ya madini ambayo ni mhimili muhimu wa uchumi wa nchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments