Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha kesho katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Songwe.
Kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka hiyo iliyotolewa leo, mvua hizo zinatarajiwa kuwa za kiwango cha wastani, huku athari zake pia zikikadiriwa kuwa za wastani.
TMA imeeleza kuwa miongoni mwa athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na uharibifu wa miundombinu katika maeneo husika.
Kutokana na hali hiyo, TMA imewataka wananchi na mamlaka zinazohusika kuchukua tahadhari mapema ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.




