Thursday, April 23, 2026
spot_img
HomeHabariJaji Chande: Oktoba 29 hayakuwa maandamano, zilikua vurugu za kupangwa

Jaji Chande: Oktoba 29 hayakuwa maandamano, zilikua vurugu za kupangwa

Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu Amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29,2025, imesema kilichotokea Oktoba 29 hakikuwa maandamano ya amani bali ghasia zilizoambatana na matukio ya uvunjifu wa amani.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Othman Chande amefafanua kuwa vijana wa makundi mbalimbali wakiwemo waendesha pikipiki, waliandaliwa na kupewa mafunzo maalumu ili kushiriki vurugu zilizosababisha uvunjifu wa amani na tishio la usalama nchi.

Jaji Chande ameeleza hayo wakati akitoa taarifa ya matokeo ya ripoti ya tume hiyo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema katika uchunguzi wa Tume hiyo, yanayodaiwa kuwa ni maandamano hayakuzingatia ibara ya 20 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria za nchi inayotaka maandamano kuwa amani na kutoa notisi kwa jeshi la polisi.

“Hi haki ya kila mtu kushiriki uchaguzi mkuu kamampiga kura au mgombea ni haki kwa mujibu wa Katiba na haipaswi kupokwa. Ghasia zilipangwa na kutekelezwa siku iliyotangazwa kisheria, hivyo kufanya ghasia siku ni kupoka haki ya wananchi wengine ikiwemo ya kupiga kura na kuchaguliwa,” amesema.

Jaji Chande amesema walishiriki wa ghasia hizo walibeba silaha za aina mbalimbali zikiwemo mawe, nondo, vipulizi, bunduki, mapanga, jambo ambalo haliruhusiwi kisheria katika maandamano.

Mbali na hilo, Jaji Chande ameeleza kuwa matukio ya Oktoba 29 yalipangwa na kufadhiliwa na kutekelezwa na watu waliopata mafunzo, huku waratibu wakitumia mbinu mbalimbali ikiwemo kuwatumia vijana waliokata tamaa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments