Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema ndani ya siku au wiki chache zijazo, Serikali yake itaundwa Tume ya Maridhiano na Muafaka wa Kitaifa, ikijumuisha wadau wote muhimu.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Alhamisi Aprili 23, 2026 wakati wa hotuba yake baada ya kupokea ripoti ya tume ya uchunguzi wa ghasia za wakati na baada ya uchaguzi.
Amesema tume hiyo, itakasimamia na kuongoza majadiliano na maridhiano katika nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi ili kuponya majeraha na migawanyiko iliyopo na kurejesha umoja na mshikamano wa kitaifa.
“Naomba niwakumbushe kuwa nia ya kuwa na tume ya maridhiano ilikuwepo hata kabla ya Oktoba 29, 2025,” amesema.




