Friday, April 24, 2026
spot_img
HomeElimuWanu: Sereikali kuimarisha elimu ya ufundi stadi

Wanu: Sereikali kuimarisha elimu ya ufundi stadi

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, anasema Serikali inaendelea kuimarisha elimu ya ufundi ili iwe suluhisho la ajira kwa vijana nchini.

Anasisitiza kuwa mwelekeo wa sasa ni kuhakikisha vijana wanapata ujuzi wa vitendo unaowawezesha kujiajiri na kuajiriwa kwa ufanisi kulingana na mahitaji ya soko la ajira.

Anaiagiza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuanzisha vituo vya umahiri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, akieleza kuwa hatua hiyo itaongeza ubora wa mafunzo na kuwajengea vijana uwezo wa kushindana katika soko la ajira.

“Tunataka vijana wetu wapate ujuzi unaokwenda sambamba na mahitaji ya soko la sasa na teknolojia mpya,” anasema.

Wanu anaongeza kuwa Serikali imezindua mtaala mpya wa mafunzo ya aluminium na ufungaji wa vioo (Aluminium and Glass Fitting with Metal Fabrication) kwa kushirikiana na sekta binafsi, hatua inayolenga kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanazingatia uhalisia wa kazi.

Anabainisha kuwa mtaala huo umejikita zaidi katika mafunzo ya vitendo ili kuwajengea vijana uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi mara baada ya kuhitimu.

Pia anasema Serikali imeelekeza kuanzishwa kwa mitaala ya aluminium katika vyuo vya VETA ili kurasimisha ujuzi wa mafundi na kuwapatia vyeti vinavyotambulika rasmi, hatua itakayowawezesha wahitimu kupata ajira kwa urahisi na kuongeza hadhi ya taaluma hiyo nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments