Monday, April 27, 2026
spot_img
HomeHabariVipaumbe 17 vya  mageuzi sekta ya sheria

Vipaumbe 17 vya  mageuzi sekta ya sheria

Wizara ya Katiba na Sheria imebainisha vipaumbele 17 ambavyo vitaleta mageuzi katika sekta ya sheria nchini kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.

Vipaumbele hivyo vimebainishwa Bungeni jijini Dodoma Aprili 24 2026 na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Juma Zuberi Homera wakati akiwasilisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Miongoni mwa vipaumbele hivyo ni pamoja na mageuzi ya mfumo wa kisheria katika haki jinai na haki madai na ujenzi wa miundombinu ya upatikanaji haki.

Dk. Homera amesema Wizara, taasisi zake pamoja na Mahakama itaendelea kuboresha utoaji wa huduma za kisheria na mifumo ya upatikanaji wa haki kwa umma kwa wakati na usawa ili kuendana na mipango ya sekta ya sheria nchini na Mipango ya Kikanda na Kimataifa ili kufikia malengo yaliyopangwa kwa kipindi husika. 

Ametaja vipaumbele vingine kuwa ni kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa mashauri ya jinai na madai, kuimarisha huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi na kuimarisha haki za binadamu na utawala bora nchini.

Nyingine ni kuimarisha masuala ya kikatiba na elimu ya uraia, luimarisha uwezo kwa wataalam wa sekta ya sheria, huduma za ufilisi na udhamini, mfumo wa utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, ulinzi wa utajiri asili na maliasilia za nchi pamoja na kulinda maslahi ya taifa pamoja na kuendeleza matumizi ya Kiswahili katika sekta hiyo.

Aidha, Dk. Homera, amebainisha vipaumbele vingine kuwa ni pamoja na  kuimarisha uwajibikaji na utendaji katika sekta ya sheria, mageuzi ya kidigitali katika sekta ya sheria na ulinzi wa watoa taarifa na mashahidi.

Ameongeza kuwa vipaumbele vingine ni mageuzi ya sheria kwa ajili ya uwekezaji na uchumi, kusimamia ajira, uteuzi, nidhamu na maadili ya watumishi wa Mahakama na kuimarisha mapitio, tafiti na tathmini za sheria ili kurahisisha utekelezaji wa DIRA, 2050.

Mpango na Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria 2026/2027 umejengwa katika muktadha mpana wa kimkakati wa taifa unaolenga kuiwezesha Tanzania kufikia hadhi mpya ya maendeleo, utulivu na ushindani wa kimataifa kuelekea maendeleo endelevu ya Taifa na mtu mmoja mmoja. 

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments