Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Zainab Katimba, amesema serikali inatarajia kuanza rasmi utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia awamu ya pili.
Akizungumza Bungeni jijini Dodoma Aprili 27, 2026, Katimba amesema kampeni hiyo itaanza rasmi Aprili 30 mwaka huu.
Ameeleza kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuwafikia wananchi katika halmashauri, kata na mikoa yote nchini, ili kuwapatia huduma za msaada wa kisheria kwa urahisi zaidi.
Hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa haki kwa wananchi na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za kisheria katika jamii.




