Friday, May 1, 2026
spot_img
HomeAfyaMchengerwa azindua boti za chanjo nchini

Mchengerwa azindua boti za chanjo nchini

Na Yasmine Protace,Kibaha

Mohamed Mchengerwa amezindua vyombo vya usafiri kwa ajili ya kuimarisha huduma za chanjo nchini katika hafla iliyofanyika Bandari ya Nyamisati mkoani Pwani.

Akiwahutubia wananchi na wadau wa afya, Mchengerwa amesema uzinduzi huo si wa vyombo vya usafiri pekee bali ni uthibitisho wa falsafa ya taifa ya kuhakikisha huduma za afya zinamfikia kila Mtanzania bila kujali jiografia.

Amesema haki ya afya haipaswi kuzuiliwa na umbali wa kijiografia, akisisitiza kuwa Serikali inawajibika kufikia mtoto yeyote anayehitaji chanjo popote alipo.

Katika hafla hiyo, amelishukuru kwa dhati Gavi, the Vaccine Alliance kwa ufadhili wa boti saba ambazo zitasaidia kusambaza na kusimamia huduma za chanjo katika maeneo ya visiwa na mwambao.

Ameeleza kuwa boti hizo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha huduma za afya, hasa katika maeneo ambayo yanakabiliwa na changamoto za kufikika, akibainisha kuwa uwekezaji huo una thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.18.

Aidha, amesisitiza kuwa kwa kuzingatia falsafa za Julius Nyerere, maendeleo ya kweli yanapaswa kuwafikia wananchi wote bila kumwacha yeyote nyuma.

Mchengerwa amehitimisha kwa kusema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Samia Suluhu Hassan itaendelea kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa na kufika kila kona ya nchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments