HomeHabariDkt Samia awasilisha ujumbe maalumu kwa Katibu Mkuu UN

Dkt Samia awasilisha ujumbe maalumu kwa Katibu Mkuu UN

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasilisha ujumbe maalumu wa Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ( UN), António Guterres na kusisitiza dhamira ya nchi kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, amani na maendeleo endelevu.

Baada ya mazungumzo yao, Balozi Kombo alimkabidhi Guterres zawadi ya kitabu kuhusu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Tanzania, kwa kutambua kuvutiwa kwa muda mrefu kwa katibu Mkuu huyo na maono, uongozi na mchango wa Nyerere katika kuhimiza amani, maendeleo na ushirikiano wa kimataifa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments