Wednesday, April 1, 2026
spot_img
HomeHabariINEC yatoa uamuzi wa rufaa 13 za kupinga uteuzi wa ubunge,udiwani

INEC yatoa uamuzi wa rufaa 13 za kupinga uteuzi wa ubunge,udiwani

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema kuwa jumla ya rufaa 33 za kupinga uteuzi wa nafasi za Ubunge na Udiwani zimewasilishwa kwake, na kati ya hizo, rufaa 13 zimefanyiwa uamuzi na Tume. Kati ya rufaa hizo 13, nane zilihusu kupinga uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi kuhusu nafasi za Ubunge, na tano zilihusu nafasi za Udiwani.

Katika kikao maalum kilichofanyika jijini Dodoma, Tume imekubali rufaa mbili na kukataa rufaa sita za Ubunge, huku pia ikikubali rufaa mbili na kukataa rufaa tatu za Udiwani.

Rufaa za Ubunge Zilizokubaliwa

Tume imekubali rufaa mbili za wagombea Ubunge, ambazo ni:

  1. Ezekiel Gabriel Katabi, mgombea Ubunge Jimbo la Muhambwe kupitia CHAUMMA, dhidi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muhambwe.
  2. Athuman Issah Henku, mgombea Ubunge Jimbo la Lkungi Mashariki kupitia CUF, dhidi ya Thomas Mgonto Kitima, mgombea Ubunge kupitia CCM.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, wagombea hao wamerejeshwa katika orodha ya wagombea Ubunge katika majimbo husika na wamepewa ruhusa ya kuendelea na taratibu za kampeni za uchaguzi.

Rufaa za Ubunge Zilizokataliwa

Tume pia imekata rufaa sita za wagombea Ubunge, ambazo ni:

  1. Msowoya Gelard Goodluck, mgombea Ubunge Jimbo la Kilombero kupitia ACT-Wazalendo, dhidi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kilombero.
  2. Innocent Gabriel Siriwa, mgombea Ubunge Jimbo la Kibamba kupitia ADC, dhidi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kibamba.
  3. David January Mhanga, mgombea Ubunge Jimbo la Mkuranga kupitia CHAUMMA, dhidi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mkuranga.
  4. Christina Gasper Mbise, mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia ADC.
  5. Cecil Fransis Akili, mgombea Ubunge Jimbo la Ndanda kupitia ACT-Wazalendo, dhidi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ndanda.
  6. Mneke Jafari Saidi, mgombea Ubunge Jimbo la Newala Vijijini kupitia CUF, dhidi ya Nawanda Yahaya Esmail, mgombea Ubunge Jimbo la Newala Vijijini kupitia CCM.

Kwa wagombea hao, Tume imekubaliana na uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo husika wa kutowateua kugombea nafasi ya Ubunge katika majimbo husika.

Aidha, kwa mrufani wa namba (vi) ya kirumi, Nawanda Yahaya Esmail, Tume imekubaliana na uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Newala Vijijini, hivyo ataendelea na taratibu za kampeni za Ubunge.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments