Thursday, March 12, 2026
spot_img
HomeMichezoMaximo aridhishwa na wachezaji wa KMC

Maximo aridhishwa na wachezaji wa KMC

Kocha wa KMC, Marcio Maximo, amesema anaridhishwa na nidhamu na ufuatiliaji wa maelekezo unaoonyeshwa na wachezaji wake.

Kauli hiyo ameitoa baada ya kikosi chake kushinda 3-2 dhidi ya Mlandege kwenye michuano ya Kagame Cup jijini Dar es Salaam.

Maximo alisema ushindi huo ni matokeo ya juhudi na mafunzo wanayoyapata mazoezini, huku akisisitiza lengo lao ni kufikia ubingwa wa michuano hiyo.

Kiungo mshambuliaji Redonatus Mussa naye aliongeza kuwa ushindi huo umeongeza morali ya timu kuelekea michezo inayofuata.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments