Thursday, March 12, 2026
spot_img
HomeMichezo'Tembo Warriors' kuanza na Kenya CECAFA

‘Tembo Warriors’ kuanza na Kenya CECAFA

Timu ya taifa ya soka kwa watu wenye ulemavu, Tembo Warriors, itaanza kampeni yake ya michuano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) dhidi ya Kenya Septemba 9 jijini Bujumbura, Burundi. Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka nchini Septemba 7.

Msemaji wa Shirikisho la Soka kwa Watu Wenye Ulemavu (TAFF), Khalid Msabaha, alisema Tanzania imepangwa kundi B na Kenya pamoja na Uganda, huku kundi A likiwa na DRC Congo, Zambia na Burundi.

Alibainisha kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na malengo makuu ni ubingwa, akiwashukuru Watanzania waliojitolea kuchangia timu hiyo kushiriki mashindano hayo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments